Tukio hilo limetokea umbari wa Kilometa nane kutoka katikati ya Jiji la Arusha, baada ya mabonge makubwa ya Moram kuporomoka, wakati watu hao wakiwa kwenye shughuli ya uchimbaji.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana, alisema tukio hilo lililotokea jana asubuhi.
Alisema tangu kutokea ajali hiyo vikosi vya uokoaji, kutoka mamlaka za ulinzi na usalama vilikusanyika eneo la tukio na kuendelea na shughuli ya kufukua udongo, kuwatafuta watu waliofukiwa.
“Lakini pia vifaa mbalimbali vya uokoaji viliwasili mara moja ili kufanikisha zoezi la ufukuaji kifusi linaenda kwa haraka na vizuri,” alisema.
Shana alisema watu watatu waliofariki walikuwa wamefunikwa na gema lililobomoka kutoka na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo na wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.
Social Plugin