Na Amiri kilagalila
Jeshi la Polisi Kupitia Kitengo Cha Usalama Barabarani Limepeleka Askari Polisi Katika Vituo 41 Vya Boda boda Mkoani Njombe Ambao Watakuwa Wakifanya Kazi ya Ulezi Kwa Madereva Hao Kwa Lengo la Kuwasaidia Kufanyakazi Hiyo Kwa Weledi na Nidhamu.
Hii Itasaidia Kupunguza Ajali za Barabarani Kwa Kuwa Elimu Itakuwa Ikitolewa Mara Kwa Mara Kwa Madereva Pikipiki Wawapo Katika Vituo Vyao Ikiwa ni Pamoja na Kuwa na Kofia Ngumu Yaani Helmet Kwa Dereva na Abiria Wake na Usafi Kwa Ujumla.
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe Kelvin Ndimbo Amezungumza na mtandao huu juu ya Hatua Hiyo huku Akisema kuwa huu ni Kwa Mujibu wa Sheria na Kwamba Tayari Tangu Askari Hao Wapelekwe Kwenye Vituo Mafanikio Yameanza Kuonekana Huku Akitoa Wito Kwa Abiria Hususani Wanawake Ambao Wanagoma Kuvaa Kofia Ngumu Kwa Kisingizio Cha Kuchafuka Nywele.
"Natoa wito na rai kwa abiria wote wanaopakizwa kwenye hizi piki piki wahakikishe wanavaa kofia kwasababu wanapanda kwenye pikipiki ambazo waendeshaji wote wamevaa hizi kofia kwa kuwa sio sale ni usalama,niwaombe abiria wavae kofia la sivyo kwa maana sheria haitasita kuwachukilia sheria wote wanaokiuka sheria"alisema Ndimbo
Madereva Bodaboda Mjini Njombe Akiwemo Kenedy Mligo na Kenedy Mkonga Wanakiri Kuwapo Kwa Mabadiliko Makubwa Tangu Askari Walezi Kuwepo Katika Vituo Vyao na Kwamba Hata Usafi Umeimarika Kwani Sasa Wanavaa Reflector Pamoja na Kuwa na Kofia Ngumu Kwa ajili Yao na Abiria Wao Licha ya Baadhi ya Akina Dada Kugoma Kuvaa Kofia Hizo.
"Askari walezi wananvyokuwepo wanafanya kweli madereva wajitambue ikiwamo kuwa na leseni,kuvaa vikinga upepo pamoja nakofia kwa kweli hii inasaidia na sisi kila wakati tunatoa elimu kwa hawa abiria wetu kwa kuwa wakati mwingine wamekuwa hata wakigoma kuvaa hizi kofia ngumu"alisema Kenedy mligo mmoja wa dereva boda boda.
Baadhi ya wanawake Akiwemo Honey Mnenuka Licha ya Kukiri Kuhofia Usafi Hasa Katika Nywele Zao Pamoja na Suala Zima la Urembo Wengine Wanashauri Sheria Kuchukua Mkondo Wake.
"Uvaaji wa kofia uwepo maana ni usalama wetu kwa hiyo ni lazima abiria kwa anayegoma lazima sheria zichukuliwe na alipe yeye na sio dereva,ila tatizo kwenye usalama unakuwa mdogo zile kofia zikiwa chafu tungeomba ziwe zinafanyiwa usafi"alisema Honey mnenuka
Neema ni Miongoni Mwa Abiria Aliyekutwa na mtandao huu Akipanda Bodaboda Ambaye Baada ya Kuvalishwa Kofia Alianza Kwa Kusita.
"Mimi siendi mbali jamani nitavaaje naenda jirani tu hapo"alisikia mmoja wa abiria wa kike akigoma kuvaa kofia ngumu.
Mtandao huu umezungumza na Baadhi ya Wanaume Mjini Njombe Akiwemo Reginald Danda na Obeid Ngailo Juu ya Suala la Kofia Ngumu Kwa Abiria Ambao Wanaeleza Umuhimu wa Kuvaa Kofia Hizo Huku Wakiwataka Akina Dada Kutumbua Thamani ya Uhai Wao Badala ya Urembo.
"Mimi nimewahi kupata ajali ya boda boda nikiwa nimevaa kofia ngumu na kofia ngumu ilipasuka huku mimi nikiwa nimepoteza fahamu siku mbili kwa hiyo kama ningekuwa sikuvaa kofia na maisha yangu yangekuwa yamekwisha,kofia hizi ni muhimu sana na watu kwa kweli waache kisingizio cha nywele ukiona nywele ni muhimu basi bora utumie gari" alisema Reginald Danda
Suala la Usalama Katika Maisha Ni Muhimu Kuliko Urembo.