Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linawashikilia watuhumiwa watano kwa kuhusishwa na tukio la mauaji ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Edina Ng'uku (50).
Akizungumza na waandishi wa habari,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Salum Hamduni amesema : Mnamo April 6 majira ya saa 11:30 kijiji cha Ikwete kata ya Lyamkena mjini Makambako mkoani Njombe lililipotiwa tukio la kuuawa kwa Edina Ng'uku (50) Mbena,mkristo na mkulima baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na kitu kizito na butu sehemu mbali mbali za mwili wake, na amechanwa na kitu chenye ncha kali sehemu zake za siri kisha kuchomwa na bua bichi la zao la alizeti "alisema kamanda Hamduni
Kamanda ameongeza kuwa mama huyo alichomwa na bua sehemu zake za siri na kutokea begani.
Amesema kuwa baada watu hao wasiofahamika baada ya kutenda kosa hilo walitoweka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.
" Aidha katika eneo la tukio mwili umekutwa ukiwa umelala upande wa kushoto ndani ya shamba lililopandwa mazao ya mahindi na alizeti ambalo linamilikiwa na Eda Nziva huku ukiwa na majeraha sehemu za kifuani upande wa kushoto karibu na ziwa lake pia ukiwa na mchubuko kwenye magoti iliyotokana na kuburuzwa chini umbali wa mita 5.5 na vilevile vimekutwa vipande viwili vya vitenge eneo tofauti,aidha mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi"alisema kamanda
Social Plugin