Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amemteua Mhandisi Rejea Samweli Ng’ondya kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA).
Uteuzi huo ulianza jana Tarehe 12.04.2019. Mhandisi Rejea Samweli Ng’ondya kabla ya uteuzi alikua Meneja wa Mamlaka ya Maji ya Makonde, Mtwara.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amemteua Mhandisi Charles Richard Mafie kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Wizara ya Maji kuanzia jana tarehe 12.04.2019.
Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Mafie alikua Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji katika Chuo cha Maji – Dar es salaam.
Kufuatia uteuzi huo, Waziri Prof. Mbarawa ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Wizara ya Maji Mhandisi Catherine Bamwenzaki kuanzia jana tarehe 12.04.2019
Mhandisi Bamwenzaki atapangiwa majukumu mengine.
Social Plugin