Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WENYEVITI 13 WA CHADEMA JIMBO LA FREEMAN MBOWE WATIMKIA CCM


Wenyeviti 13 wa Vitongoji katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro ambalo linaongozwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), wameitikisa tena ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini, baada ya kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

Kundi hilo la wenyeviti hao wa vitongoji, linaivuruga ngome hiyo, huku ikiwa imepita miezi saba tangu Wenyeviti wa Serikali za Vijiji 19 katika Halmashauri ya Wilaya hiyo ambao wanatoka na Chadema, kubwaga manyanga na kujiunga na CCM, Septemba 6 mwaka jana.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kupokea barua za kujiuzulu kwa wenyeviti hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Yohana Sintoo alithibitisha kupokea barua za kujiuzulu kwa wenyeviti hao 13 jana asubuhi.

Aliwataja wenyeviti waliojiuzulu na vitongoji vyao kwenye mabano kuwa ni Gladson Swai (Bomani), Ruyandumi Kimaro (Makiweru-Uswaa), Beda Msofe (Lembeni B-Rundugai), Ndemael Massawe (Nure-Ng’uni), Leonard Urassa (Njoro Chini-Shirinjoro) na Raymond Mushi (Nkwelengy-Nronga).

Wengine ni Filbert Usiri (Nkwamandaa-Nronga), Eliatosha Lema (Maaseni-Nronga), Majisia Paul (Ngulujuu-Chemka), Nimkaza Mhando (Kikuletwa-Chemka), Gasper Mwasha (Boma Kati-Kware), Walter Swai (Masamu-Uswaa) na Majinsi Nyange (Lembeni A-Rundugai).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com