Wizara ya Mambo ya Ndani imeliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh 921.2 bilioni mwaka wa fedha 2019/2020.
Kati ya fedha hizo, Sh889.3 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida,Sh372.2 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo na ShSh517 bilioni za mishahara.
Fedha za miradi ya maendeleo ni Sh 31bilioni na kati ya fedha hizo za maendeleo, Sh21.5 bilioni ni fedha za ndani na Sh10.4 bilioni ni fedha za nje.
Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni leo Jumatano Aprili 24, Waziri wa Wizara ya Mmabo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema vipaumbele vya bajeti hiyo ni kudumisha usalama wa raia na mali zao kwa kufanya doria, misako na operesheni mbalimbali.
Vingine ni kuboresha mazingira ya ofisi na makazi ya askari na watumishi raia na kuwaongezea ujuzi watumishi raia na askari kwa kuwapa mafunzo ya ndani na nje ya nchi.
Lugola amesema vipaumbele vingine ni kuendelea kutekeleza mkakati wa jeshi la magereza wa kujitosheleza kwa chakula, kuendelea kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu kwa kuimarisha utendaji wa shirika la uzalishaji mali la jeshi hilo
Social Plugin