Mwanadada maarufu kutoka nchini Uganda Zari Hassan 'Zari the Bosslady' ameanza uhusiano mpya wa mapenzi zaidi ya mwaka mmoja tangu atangaze kukamilika kwa uhusiano wake na nyota wa Bongo, Diamond Platnumz.
Imeabainika wazi sasa Zari mwenye umri wa miaka 38 amepata mchumba mpya ambaye anachukua nafasi ya mpenzi wake wa zamani Diamond.
Akipakia picha ya jamaa huyo anayemwita Mr. M, mrembo huyo alimmiminia jumbe za sifa akifichua kuwa, amejawa na furaha moyoni mwake kwani mahali yupo kwa sasa amepata uridhisho.
"Umenifunza mengi, nayathamini maisha kutokana na unyenyekevu wako. Hata baada ya kupata watoto watano kutoka kwa wanaume wengine, bado ulinipenda vivyo hivyo," Zari alisema.
Akitangaza uhusiano wake mitandaoni, Zari alifichua kuwa mchumba wake mpya amekubali kuishi naye pamoja na wanawe watano.
"Nakupenda sana Mr. M, sio kwa sababu ya zawadi unazonipa kila kuchao, hayo yote nimeyashuhudia na hata zaidi. Lakini kwa ajili ya roho yako, nafsi yako na hisia ambazo unanipa mimi na wanangu," aliongeza.
" Uamuzi wako unaashiria ujasiri Mr .M. Nina watoto watano, nina umri wa miaka 38...kweli nakuthamini. Nakupenda Mr. M," mrembo huyo alifichua.
Mrembo huyo ambaye pia ni mfanyabiashara alisikitika jinsi alivyojibidiisha kuyaimarsiha maisha ya wachumba wake wa zamani, ambao , kulingana na yeye hawakumthamini wala kumuonesha mapenzi alivyostahili.
"Najitolea kwa vyovyote vile ili kuwajenga bwana zangu, kwa kawaida mimi sio mwanamke wa kupokea tu kutoka kwa wachumba ninaohusiana nao bali natumia kidogo tulicho nacho ili kupata baraka maradufu," alisema.
Februari 14, 2018, mwanadada huyo alitangaza kukamilika kwa uhusiano wao wa miaka mitatu na Diamond, akitaja uzinzi na vile vile kukosewa heshima kama sababu kuu zilizowatenganisha.
Hata hivyo, Diamond Platnumz alijinyakulia kipusa mwingine Tanasha Oketch ambaye ni mtangazaji.
Aidha, Zari alijaaliwa watoto wawili na Diamond huku akipata wavulana watatu na marehemu Ivan Ssemwanga.
Social Plugin