Mzazi mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady, amefunguka baada ya msanii Diamond kuongea mengi kuhusu mahusiano yao yaliyopita ndani ya kituo chake cha redio cha Wasafi FM jana, April 23, 2019.
Diamond alifunguka mambo mengi ikiwemo Zari kumsaliti kwenye mahusiano, kuhusiana na kutoa sapoti kwa wanaye, na mambo mengine yaliyokuwa yanawahusu walipokuwa kwenye mahusiano.
Zari amejibu kwa kusema; “Sasa yale magoti mpaka Sauzi yalikuwa ya nini? Kule kuomba msamaha kwote kwa radio kwa nini? Kwani umekuwa comedian sasa? Usinichafulie maisha bro. Yameisha zamani kubali tu. Kiki zimekuwa ngumu mjini. Niheshimu tafadhali nakulelea watoto tena vizuri.
"Mimi sijawahi kuchepuka wakati nipo naye na ninajiapiza kama nimewahi kufanya hivyo basi lolote liwatokee watoto wangu.
“Sasa kama mtu amewahi kuikana damu yake kuna uongo gani mwingine anaweza kuacha kusema? Ni vyema kukiri makosa yako na kuyatumia kukua, bado unayo nafasi,” Amesema Zari
Social Plugin