Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada
Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada
Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa na wanafamilia baada ya kumtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada
Stempu iliyowekwa picha ya Jellah Mtagwa
Mchezaji kandanda wa zamani wa Taifa Stars na Yanga na Pan African Jellah Mtagwa yupo kitandani akiugua kiharusi na anahitaji msaada wa matibabu pamoja na kujikimu kimaisha.
Mtagwa, ambaye hivi sasa amepooza nusu ya mwili wake, anaishi Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam pamoja na familia yake akiwa hana hili wala lile kutokana na maradhi hayo na ufukara.
Wadau na mashabiki wa mpira wa miguu wameelezea masikitiko yao kwa hali kama hiyo kumkumba aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa Stars ambaye picha yake iliwekwa kwenye stempu kutokana na mchango wake uliotukuka kwa nchi.
Wengi wanahoji endapo kama Shirika la Posta lilimlipa mchezaji huyo mrabaha wa kuwekwa sura yake mwenye stempu, na kama Shirikisho la Mpira nchini (TFF) wana taarifa zake na kama wanamsaidia kwa chochote.
Hivi tunavoongea umoja wa wachezaji soka wa zamani (UMSOTA) wameanzisha harambee ya kumsaidia mwenzao huyo kwa kuchangishana ili kumsaidia.
Tayari umoja huo umetoa ombi la msaada kwa wasamaria wema kumsaidi Jellah Mtagwa kwa kutangaza namba yake ya simu Namba 0755 693330 kwa yeyote atakayeguswa.