AJALI YA BASI, HIACE YAUA MWANAFUNZI BABATI


Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa ajali kati ya basi la Kampuni ya Mtei na basi dogo aina ya hiace katika eneo la Himiti mjini Babati, na kupelekea kifo cha mwanafunzi wa Shule ya Msingi Silver  aliyefahamika kwa jina la Osiligi Paul (3).


Amesema mwalimu wa Shule ya Silver ambayo zamani ilikua ikiitwa Deborah, Francis Mollel (36) amejeruhiwa kwenye ajali hiyo pamoja na mwanafunzi Lightness Emmanuel (6) na wakala wa Mtei Paul Shilala (28) wamepata majeraha na wapo Hospitali ya Mrara mjini Babati.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la Mtei kuipita gari nyingine bila tahadhari na kugongana na basi dogo kwenye barabara hiyo ya Babati-Kondoa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post