Rais Felix Tshisekedi amemteua Profesa Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa Waziri Mkuu Mpya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Uteuzi huo umefanyika muda mfupi uliopita baada ya hapo awali waziri mkuu aliyekuwepo Bruno Tshibala, kujiuzulu.
Sylvestre amewahi kushikilia nyadhifa tofauti serikalini.
Yeye ni mfuasi wa chama cha rais wa zamani nchini Congo Joseph Kabila - PPRD.
Raia wa Congo wamesubiri zaidi ya miezi mitatu, pasi kuwa na waziri mkuu mpya.
Mwanasiasa huyu mwenye umri wa miaka 78 ambaye pia ni miongini mwa viongizi wa chama cha Joseph Kabila, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya reli Congo.Aliwahi kutumika chini ya utawala wa Mobutu Seseko kama mshauri wake wa masuala ya uchumi.