Mwanafunzi Magreth Kayuni (15) wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Vwawa iliyopo wilayani Mbozi mkoani wa Songwe, amekutwa amejinyonga jikoni leo asubuhi kufuatia adhabu ya kupigwa na bibi yake baada ya kuiba begi la mwanafunzi mwenzake.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mdogo wa marehemu, Abraham Kalinga, amesema mapema leo asubuhi walipoamka bibi yao alimuagiza apike maharage, huku yeye akifanya kazi ya kufagia uwanja, marehemu Magreth Kayuni baada ya kupika maharage aliaga kuwa anaenda kuchota maji na ndipo alipofikia uamuzi wa kujinyonga.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Seleman Mgala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limewastua wakazi wa eneo hilo ambapo amesema tukio kama hilo halijawahi kutokea mtaani hapo na hiyo ni mara ya kwanza.
Social Plugin