Jamaa watatu waliopatikana na kosa la kuiba Biblia 500 kutoka kituo cha utafsiri wa vitabu cha Bible Translation and Literacy wamepigwa faini ya Ksh 500,000 kila mmoja nchini Kenya.
Jamaa hao ambao ni Reuben Rogoi Maina, John Mapesa Andulu na Josephat Gatheru wamefikishwa mahakamani na kupigwa faini ya KSh 1.5 milioni kwa kosa hilo na wamekanusha mashtaka ya wizi huo na kuachiliwa kwa dhamana.
Kulingana na Gazeti la Taifa Leo, watatu hao wanakisiwa kuiba Biblia hizo kutoka kwa kituo cha utafsiri wa Bibilia (Bible Translation and Literacy (EA) mtaani Upperhill, Nairobi.
Mahakama iliarifiwa kuwa watatu hao walikuwa wamelaghai kituo hicho kwa kuandika hundi bandia ya kulipia bei ya vitabu hivyo huku wakijifanya ilikuwa halali.
Baada ya kugundua ukora wa waili hao, kituo hicho kilitoa taarifa kwa polisi na kukamatwa kwa watatu hao. Kesi hiyo itatajwa baada ya wiki mbili.