Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umewasilisha mpango kazi wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), unaotekelezwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) hapa nchini kupitia Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC).
Mpango kazi huo umewasilishwa leo Mei 20, 2019 jijini Dodoma kupitia kikao kazi kilichowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni 23 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Akiwasilisha mpango kazi huo, Victor Maleko ambaye ni Afisa Programu kutoka UTPC amesema pamoja na mambo mengine, umelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mitandaoni kuzifahamu sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya Takwimu 2015, Sheria za Huduma za Vyombo vya Habari 2016 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 ili kuripoti kwa weledi habari za utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC), Claude Gwandu amewataka washiriki wa mradi huo kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha unafikia malengo yaliyokusudiwa na kwamba chama hicho hakitakuwa tayari kuona mradi unakwamba kutokana na baadhi ya washiriki kutowajibika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers/ Online TV), Midraji Ibrahim amesema ili mitandao ya kijamii iendelee kuwa na manufaa katika jamii, lazima waandishi wa mitandao hiyo waweke habari zenye maudhui bora ikiwemo utetezi na uchechemuzi wa haki za binadamu kupitia takwimu sahihi.
Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT ambapo ulianza mwaka jana 2018 ukitarajiwa kufikia tamati mwaka 2022.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha Kadama Malunde (Malunde 1 Blog), William Bundala (Kijukuu Blog), Merina Makasi (Ngasa TV), Mohamed Zengwa (Global TV), Eliya Mbonea (Mtanzania Digital), Midraji Ibrahim (Sub Editor Mwananchi Digital), Mika Ndaba (Ayo TV), James Range (Sub Editor/ Programme Manager Global TV), Frankius Cleophace (Cleo24 News and Dar Mpya), Asha Shabani (Asha Shabani TV), George Binagi (Binagi Media Group), Albert G. Sengo (GSengo Blog).
Wengine ni Francis Godwin (Dar Mpya Blog/ Matukio Daima Blog), Abubakar Kisandu (Kisandu Zenji Blog), Rashid Said Rukungu (Rukungutz Blog CG Online Tv), Editha Karlo (Correspondent (Michuzi Blog and Malunde Blog), Joseph Mwaisango (Mbeya Yetu Online TV), Bakari Chilumba (Correspondent Dar Mpya Blog, Millard Ayo, Mpekuzi na Muungwana), Abdulaziz Ahmed (Lindi Yetu Blog na Lindi yetu Online TV), Gabriel Kilamlya (Dar 24 Blog), Ibrahim Said Limala (Correspondent Global TV online), Clavery Christian (Muungwana Blog) pamoja na Hamza Mashore (Ruvuma TV).
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akiwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (Data Drive Advocacy- DDA) kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers).
Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC), Claude Gwandu akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Arusha Pres Club (APC), Claude Gwandu kwenye kikao kazi hicho.
Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema.
Mwenyekiti wa kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers/ Online TV), Midraji Ibrahim (aliyesimama), akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha washiriki 23 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia mpango kazi wa utekelezaji Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni (Bloggers/ Online TV) nchini Tanzania.
Washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Maafisa Programu wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Social Plugin