Watu 143 wamenusurika kifo baada ya ndege aina ya Boeing 737 waliyokuwa wanasafiria kutoka Cuba kwenda Kaskazini mwa Florida, Marekani kutumbukia mtoni.
Katika tukio hilo lililotokea Ijumaa Mei 3 jioni hakauna mtu yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.
Ndege hiyo ya kukodi iliyokuwa inatua katika uwanja wa jeshi wa Jacksonville ikitokea Guantamano Bay ikiwa na abiria 136 na wafanyakazi saba, iliacha njia ya kutua na kuingia katika mto wa St Johns.
Vikosi vya uokoaji majini viliwahi na kuwaokoa watu wote na ndegehiyo ilikuwa katika maji ya kina kifupi haikuwa imezama.
“Kila mtu katika ndege hiyo alikuwa hai,” lilisema shirika la habari la NAS katika twitter na kwamba watu 21 walipelekwa hospitalini na hali zao hazikuwa mbaya.
Picha pekee iliyotolewa ilionyesha nembo ya shirika la Miami Air International, lakini shirika hilo halikujibu ujumbe wa wanahabari.
Mkazi wa jirani na eneo hilo, Loz Torres alilieleza Florida Times-Union kwamba alisikia mlio kama wa bunduki akiwa nyumbani kwake katika eneo la Orange Park karibu kilometa 8 Kusini mwa eneo ndege hiyo ilipotumbukia mtoni.
Baadaye alikwenda eneo la maduka, mahali ambapo polisi na vikosi vya zimamoto ilikuwa vimeweka kambi kwa ajili ya kutoa msaada.
“Kwa kweli sijawahi kuona jambo kama hili,” alisema.
Meya wa Jacksonville, Lenny Curry aliandika katika twitter kuwa vikosi vinaendelea kudhibiti mafuta ya ndege katika mto huo.
Kikosi cha zimamoto cha Jacksonville kiliandika kwenye twitter kuwa karibu asilimia 90 ya waokoaji wamewahi katika eneo la tukio na kuwa idara yake ya uendeshaji ilikuwa imefanya mafunzo ya jambo kama hilo siku hiyo ya Ijumaa.
Vikosi vya jeshi la majini na dharura vilikuwa eneo hilo kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la maji.
Ndugu wa abiria waliokwenda kuwapokea abiria hao walielezwa wawe tayari, lakini mamlaka hazikutoa taarifa kwa nini na kwa namna gani ndege hiyo iliacha njia ya kutua.
Social Plugin