Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Jumatano Mei 8, 2019 ameikana video ya ngono inayosambaa mitandaoni kwa kusema kuwa video hiyo imetengezwa kwa kuchukua sehemu ya mwili wake na mwili wa mtu mwingine.
Gwajima amesema mkono unaooneka katika video ile sio wa kwake, bali ni wa Baunsa lakini akakiri kuwa kifua kilichotumiwa ni picha yake ambayo aliipiga miaka 10 iliyopita akiwa na familia yake.
==>>Hapo chini ni nukuu ya baadhi ya maneno aliyosema
"Mimi nasema siwezi kufa hata kutekwa kilichotokea juu yangu ni mpango wa kunichafua tu, tutavishinda hivi vita mapema na kwa ukubwa.
"Ukiangalia ule mkono ni wa baunsa, sio mkono wangu mimi, hata kwa kutumia akili tu, ni nani arekodi video akiwa anajamiana halafu aisambaze yeye?
"Picha ya kifua wazi iliyotumika na kusambazwa ni picha ya familia niliyopiga nikiwa na mke wangu na watoto wangu. Na sio vibaya kupiga picha kifua ukiwa na familia. Na picha ile nilipiga zaidi ya miaka 10 iliyopita.
"Nimetuma taarifa TCRA wamtafute huyo mtu aliyepost video zile na wakala wa huyo aliyetuma taarifa hizo yupo hapa kwenye mkutano huu.
"Wataalamu walitaka kuja kuwaeleza namna video ile ilivyotengenezwa, nimekataa nikawaambia haina haja, huyo aliyetengeneza ameonyesha mimi ni mwanaume wa Kisukuma kamili, kuzaa naweza, nina watoto.
"Nafuatilia ni nani ambaye anatengeneza hizi video lakini ambaye anapost yupo hapa Tanzania ntaendelea kuwapa updates na ikifika Jumapili mtu huyu mwenye mkakati huu ovu asipojitokeza ntamuangukia jumla jumla.
"Rais alishahoji kuhusu kutekwa kwa MO Dewji lakini hadi leo hakuna kitu, sio Serikali inayohusika kwenye utekaji, bali kuna mtu mmoja mpumbavu au kikundi cha watu wanataka kuharibu taswira ya nchi.
"Hata kama video ile ilikuwa ni ya kweli, kutokana na kuwa aina ya video ile haipaswi kuonwa na kila mtu, basi unajua moja kwa moja kuwa nia ya huyo mtu si nzuri. Sasa mimi simpigi mtu aliyeko mbele, nilikaa kimya nimjue kwanza aliyeko nyuma, ili nimpige yeye
"Uchaguzi unakaribia mwaka 2020, sasa kuna watu wanahofu kwamba ninaweza kuwa na sauti nikawazidi hivyo wanajaribu kuniharibia. Niwaambie tu, ndio wananiongezea sauti, na wamethibitisha kuwa mimi ni mwanaume wa kweli.
"Amewathibitishia watu kwamba Mimi ni Mwanaume kamili, kwamba kufanya tendo la ndoa naweza kufanya sawa sawa, kila Mwanaume anafanya tendo la ndoa, tofauti hufanyia chumbani.
"Mimi nilijua Vita imeisha kabisa sababu mnapomaliza ugomvi hakuna sababu ya mvutano kuendelea Kila mtu anatakiwa kuweka silaha zake chini iwe mundu iwe panga" Amesema Askofu Gwajima
Social Plugin