Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Tano wa Bunge la Afrika (Pan - African Parliament ulioanza Mei 6,2019 umefungwa leo Ijumaa Mei 17,2019 katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika,yaliyopo Midrand jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Kupitia mkutano huo Wabunge wa Bunge la Afrika walijadili masuala mbalimbali kuhusu bara la Afrika ambapo Kauli mbiu ya Bunge la Afrika mwaka huu ni "2019 mwaka wa Wakimbizi,wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani : Kuelekea kupata masuluhisho ya kudumu katika kulazimishwa kuhama makazi katika Afrika".
Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akifunga mkutano wa bunge la Afrika leo Ijumaa Mei 17,2019 jijini Johannesburg,Afrika Kusini . Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Rais wa PAP, Mhe. Roger Nkodo Dang akifunga mkutano wa bunge la Afrika. Kushoto ni Makamu wa Kwanza wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (Tanzania) ,akifuatiwa na Makamu wa pili wa rais wa bunge la Afrika,Mhe. Haidara Aichata (Mali), Makamu wa tatu wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Bouras Djamel (Algeria) na Makamu wa nne wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe.Chief Charumbira (Zimbabwe).
Viongozi wa PAP wakiwa wamesimama wakati wa kuimba wimbo wa Umoja wa Afrika wakati wa kufunga mkutano wa bunge la Afrika leo Mei 17,2019. Katikati juu ni Rais wa PAP, Mhe. Roger Wa kwanza kushoto chini ni Makamu wa Kwanza wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (Tanzania) ,akifuatiwa na Makamu wa pili wa rais wa bunge la Afrika,Mhe. Haidara Aichata (Mali), Makamu wa tatu wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Bouras Djamel (Algeria) na Makamu wa nne wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe.Chief Charumbira ( Zimbabwe).
Wabunge wakiimba wimbo wa Umoja wa Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog