Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA YATISHIA KUTOA TAARIFA YA KUTEKWA MDUDE POLISI WAKINYAMAZA


 Chadema imelitaka Jeshi la Polisi kueleza kilichomtokea Mdude Nyagali maarufu Mdude Chadema aliyepatikana jana usiku baada ya kutekwa kwa siku tano.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema amesema leo, Mei 9, 2019 kuwa polisi isipotoa taarifa hiyo mapema, Chadema wataeleza.

Mrema amesema kwa sasa hawataki kuingilia kazi ya polisi kwani wanaamini watafanya kwa uadilifu, lakini ni muhimu wakaueleza umma kinachoendelea.

“Wameshamhoji Mdude na tuna taarifa kuwa katika uchunguzi wao kuna watu wengine kule Songwe wamehojiwa, basi waondoe hii taharuki kwa kuweka wazi angalau kidogo kuhusu suala hili,” amesema Mrema.

Amesema, “wakishindwa kufanya hivyo kwa haraka, basi sisi hatutanyamaza tutaweka wazi kile ambacho Mdude aliwaambia polisi maana wakati anahojiwa viongozi wa chama walikuwepo.”
Na Elizabeth Edward, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com