Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuripoti taarifa za matokeo ya tafiti zinaofanywa na taasisi mbalimbali ili wananchi waweze kupata taarifa.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Bakari Msangi kwenye Mafunzo yaliyohusisha wana habari,Watafiti na wawakilishi kutoka SIDO na VETA yanayofanyika katika ukumbi wa VETA Mtwara.
Dkt. Msangi ameongeza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza zaidi habari za Michezo,Burudani na Siasa kuliko Habari za Utafiti ambazo zingesaidia wananchi kupata Elimu kuhusu mambo mbalimbali yatokanayo na tafiti ikiwemo kilimo
Amefafanua kuwa ni vema kuripoti matukio na matokeo ya Tafiti kwa lugha rahisi na zinazoeleweka kwa wananchi kutokana na mahitaji husika ya habari
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameanza jana yameandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) lenye jukumu la kuhamasisha, kuratibu, kuhifadhi, kusambaza na kuendeleza tafiti chini.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Bakari Msangi akifungua mafunzo hayo.