Na Amiri kilagalila
Kaimu mkuu wa mkoa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye pia ni mkuu wa Wilaya Nyamagana amefagilia serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna ilivyoonesha umahiri mkubwa wa kuibua miradi inayotatua changamoto za watu wote katika nyanja ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, anga, reli, bandari, kilimo na mifugo.
Dkt. Nyimbi amebainisha hayo akifunga kongamano la kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu tano katika miaka minne mkoani Mwanza.
Ambapo amepongeza umahiri wa uwasilishaji wa mada mbali mbali zilizotolewa katika kongamano, umakini wa ichangiaji Mada kwa washiriki wote. Dkt. Nyimbi akihitimisha kwa kuomba waandaji wa kongamano hilo taasis ya Sautu ya Jamii Tanzania mwaka ujao kuuongeza mada itakayo pima mafanikio kwa kuakisi usawa wa kijinsia.
Akitoa salamu za Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana, Bi Florah Magabe amepongeza umahiri wa uongozi wa Magufuli kwa kutekeleza ahadi zote alizozitoa katika Ilani yake ya Uchaguzi kwa zaidi ya 75%.
Kadharika amesifia uongozi huu umewezesha wilaya ya Nyamagana kupata ongezeko ya 100% ya madawa na vifaa tiba, ujenzi wa Zahanati tano mpya pamoja na kituo cha afya chenye hadhi ya hospitali ya wilaya.
Bi. Magabe ameomba mwaka ujao kongamano hilo lifanyike wazi kuongeza idadi ya washiriki maana uongozi wa Magufuli kwa kushirikiana na Mhe. Mabula wilayani Nyamgana serikali imewezesha ujenzi wa madaraja mawili ambayo yalijengw enzi za ukoloni zitakazo unganisha wilaya ya Magu, Kwimba na Misungwi.
Kadharika amefafanua namna ambavyo Nyamagana imejidhatiti kutatua uhaba wa maji kwa miaka 20 ijayo kwa serikali kwa kutoa fedha kwa miradi mikubwa ya miwili ya maji, ujenzi wa barabara zote za mjini kwa kiwango cha rami pamoja na kujenga barabara za moramu na mawe.
Kongamano hilo la pili kufanyika kitaifa limeandaliwa ba taasis ya Sauti ya Jamii Tanzania na kuwakutanisha wadau wa maendeleo ambapo mada mbali zilitolewa ba TAKUKURU, TRA, NIDA, Taasis za fedha, Wanazuoni pamoja na mfuko wa Pembejeo.
Social Plugin