Kuafutia kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi kilichotokea Mei 2 huko Dubai, familia kupitia kwa mwanasheria wake Michael Ngalo, imeweka wazi ratiba ya msiba.
Akiongea leo Mei 3, 2019 nyumbani kwa Dr. Mengi, Ngalo amesema mwili utawasili nchini Jumatatu ya Mei 6, 2019 na kupelekwa katika hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Aidha Ngalo ameongeza kuwa Jumanne ya Mei 7, 2019, mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwaajili ya watu wote kuuga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake.
Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame ambako Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la Kisereni (KKKT).
Social Plugin