Na.Faustine Gimu Galafoni,Kutoka Jijini Dodoma.
Bunge limeelezwa kuwa ,Serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi halmashauri 3 hapa nchini kutokana na kukidhi vigezo vya mapato kujitosheleza.
Hayo yamesemwa leo Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa TAMISEMI ,Mhe.Seleman Jafo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Msalala Kahama Ezekiel Maige aliyehoji,lini mji wa Kahama utapandisha kuwa hadhi kuwa Manispaa baada ya kutimiza vigezo vya mapato kujitosheleza pamoja na Isaka kupandishwa hadhi ya Mji.
Akijibu Swali hilo,Waziri wa TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema Serikali inatambua maeneo matatu hapa nchini ambayo serikali ipo katika mchakato wa kupandisha hadhi kuwa Manispaa kutokana na kukidhi vigezo vya kujitosheleza kimapato.
Mhe.Jafo ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga,Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani na Halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita na muda wowote kuanzia sasa maeneo hayo yatapandishwa hadhi kuwa Manispaa pindi mchakato utakapokamilika.
Social Plugin