Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (CHADEMA), amepinga hoja ya baadhi ya wabunge wenzake wanaotaka nyongeza ya Sh, 50 kwa kila lita ya petroli na dizeli ili ziende kusaidia Mfuko wa Taifa wa Maji.
Heche ametoa kauli hiyo bungeni leo Mei 3, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Maji, ambapo amesema tozo hiyo sio dawa ya suluhisho la kupatikana kwa fedha za miradi ya maji kwani hata bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2018/2019 inaonyesha fedha zilitolewa ni pungufu.
“Mheshimiwa Mwenyekiti siungi mkono kuendelea kuwanyonga wananchi kwa kisingizio cha kuongeza fedha kwenye maji wakati hata tulizowaidhinishia hazijatoka.
“Niwaombe wabunge tuibane serikali itoe fedha, kila kitu tutakuwa tunaongeza kwenye mafuta hadi lita ifike Sh, 4, 000?,” amehoji Heche.
Social Plugin