Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa leo Jumatano April 8, 2019 amezungumzia tena sakata la video ya ngono inayodaiwa kuwa ya Askofu Josephat Gwajima na kusema kuwa Askofu huyo kwa sasa sio mtuhumiwa, bali ni muhanga aliyeathiriwa na tukio hilo.
Amesema kwa kushirikiana na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa video hiyo ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
"Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limeanza uchunguzi wa video hiyo mara moja na linapenda kuwapa taarifa wananchi (kuwa) Gwajima siyo mtuhumiwa, ni muathirika wa tukio hilo kwani tukio hilo linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa nia ya kutaka kuharibu heshima yake kwa jamii na waumini," amesema Mambosasa.
Mambosasa ametoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza video hiyo kwa maelezo kuwa ni kosa la jinai na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu kwani uchunguzi unaendelea ili kubaini aliyeisambaza na lengo la kufanya hivyo.
Social Plugin