Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimpokea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika “Pan- African Parliament” yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini leo Mei 7,2019.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimkaribisha ofisini Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang (katikati) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele.
Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akizungumza jambo wakati wa majadiliano hayo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa majadiliano yake na Viongozi wa Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu hali ya uchaguzi Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete ambaye anaongoza Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 akiongoza kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi huo nchini Afrika Kusini.
Kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini kati ya Viongozi wa Bunge la Afrika na timu ya waangalizi ya Umoja wa Afrika inayoongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete kikiendelea.
Waheshimiwa Mabalozi kutoka Kenya,Nigeria wa kiongozwa na Balozi Naimi Aziz wa kwanza kulia anayeiwakilisha Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika ambao wameambatana na Mheshimiwa Kikwete.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (wa tatu kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2019 nchini Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akitembelea ukumbi wa Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akipiga picha ya kumbukumbu ofisini kwake na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
****
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete ametembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika “Pan- African Parliament” yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Dkt. Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika wa Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 amepokelewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele leo Jumanne Mei 7,2019.
Amelipongeza Bunge la Afrika kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusimamia Demokrasia, Utawala na Masuala ya Ulinzi na Usalama barani Afrika.
“Mimi nilikuwa miongoni mwa Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao tulikutana kule Sirte Libya kuandaa kanuni za kuanzishwa kwa Bunge la Afrika,hivyo ninayo furaha kubwa kuona hatua kubwa ya maendeleo ya bunge,Nawapongeza sana Rais na Makamu wa Rais kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuendeleza bunge hili na Waafrika wote tunawatagemea”,amesema Dkt. Kikwete
“Leo na timu yangu ya uangalizi ambao tupo hapa Afrika Kusini kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi mkuu wa mwaka huu,na ninashukuru miongoni mwa timu yangu wabunge wa bunge la Afrika ni miongoni mwa wajumbe wangu,nawapongeza sana Bunge la Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kusimamia demokrasia”,ameongeza Dkt. Kikwete.
Kwa upande,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele amemshukuru na kumpongeza, Mheshimiwa Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa bara la Afrika kwenye nyanja za afya,elimu na demokrasia.
"Sisi viongozi vijana tuna mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wako mkubwa kwenye masuala ya uongozi na siasa za kimataifa, binafsi nakushukuru sana kwa malezi yako ambapo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nimeweza kufika hapa nilipo kiuongozi",amesema Mhe. Masele.
Aidha amemuahidi Mheshimiwa Kikwete kuwa Bunge la Afrika litatoa ushirikiano wote unaohitajika ili kuweza kutimiza majukumu yake katika uangalizi wa uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019.
Na Kadama Malunde - Johannesburg,Afrika Kusini
Social Plugin