Na Shushu Joel, Chalinze.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa kata,vijiji na vitongoji wa kata hiyo alisema kuwa amefanya maamuzi hayo ya kuanzisha ujenzi wa shule hiyo kutokana na changamoto zinazowakabili wazazi/walezi na wanafunzi kwa kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata elimu ya shule ya msingi huku wazazi kwa ajili ya masuala ya kimaendeleo.
Alisema kuongezeka kwa watu katika hilo eneo la Choza kimepelekea kuhitajika kwa haraka kwa huduma za kijamii ili kuendana na mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.
"Saruji niliyotoa ni uanzilishaji wa ujenzi wa shule hiyo lakini si kwamba ndio mwisho wa utoaji wangu wa mahitaji katika ujenzi huo bali ni kama kiongozi wa mfano ili hata wananchi wanapoambiwa wachangie wasisite" ,alisema Ridhiwani Kikwete
Aidha aliongeza kuwa wananchi ndiyo nguzo ya maendeleo hivyo wanapoamua jambo lolote lile la kimaendeleo ni lazima lifanyike kutokana na umoja, nguvu na mshikamano wao katika ufanikishaji wa maendeleo katika eneo husika.
Pia mara baada ya kutoa mifuko hiyo ya saruji Ridhiwani aliwataka viongozi wa eneo hilo kutafuta eneo jingine kubwa lenye kufaa ujenzi wa zahanati ili pia Choza pajengwe zahanati.
Pia amewataka wananchi wa Choza kujitokeza kwa wingi katika kuhamasishana juu ya maendeleo kwani serikali inatambua makusudi yao.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Ubena Zomozi Nicholaus Muyuwa amempongeza Mbunge huyo kwa uanzilishi wake wa kutoa saruji kwa lengo la ujenzi wa shule katika eneo hilo ili kuwaondolea changamoto watoto wa maeneo hayo.
Aidha amemhakikishia Ridhiwani kuwa saruji hiyo itatumika kama ilivyokusudiwa kufanyika kwani hata wao walikuwa wakilifikiria tu lakini Mbunge huyo kafanya kweli.
Naye Cosmos Alphonce ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kaloleni ameshukuru kwa mchango uliotolewa na mbunge na kumtaka aendelee na moyo huo wa kujitolea kwa wananchi wake.
Aliongeza kuwa kujengwa kwa shule katika eneo hilo kutaondoa changamoto ya watoto wa eneo hilo kutembea kilometa nyingi.