Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KOREA KASKAZINI YATAKA IRUDISHIWE MELI YAKE ILIYOKAMATWA NA MAREKANI


Korea Kaskazini imetaka irudishiwe meli yake ya mizigo iliyokamatwa na Marekani wiki iliyopita kwa kukiuka vikwazo vya kimataifa ikisema "kitendo hicho kinakwenda kinyume na sheria na kinakera mno". 

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kaskazini ameikosoa hatua hiyo akisema inapingana moja kwa moja na dhamira ya tamko lililotiwa saini na kiongozi wake Kim Jong Un na Rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano wao wa kilele wa kihistoria nchini Singapore mwezi juni. 

Siku ya Ijumaa Wizara ya sheria ya Marekani ilisema imeikamata meli ya mizigo ya Korea Kaskazini kwa jina MV Wise Honest, mwaka mmoja baada ya kushikiliwa nchini Indonesia ikisema ilihusika na shughuli haramu zinazokiuka vikwazo ilivyowekewa.

 Ilikuwa mara ya kwanza kwa meli ya Korea Kaskazini kukamatwa na Marekani kwa kukiuka vikwazo, baada ya miaka kadhaa ya mchezo wa paka na panya baharini ambapo meli za Korea zilijificha kwa kutumia bendera bandia na kuzima mitambo ya kuzifuatilia ili keupuka kugunduliwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com