Lile tamasha kubwa la Muziki wa Injili Mkoani Mwanza Liitwalo Lakwetu Concert linatarajia kufanyika kwa Kishindo Jijini humo tarehe 9 Juni Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Famara Promotion waandaji wa Lakwetu Concert Bi Catherine Mniko alisema kuwa tamasha la Mwaka huu litakuwa kubwa kutokana Maandalizi yaliyofanywa na Kamati ya uratibu.
Catherine alisema Kamati imejiandaa vya kutosha kuratibu kila kitu na wanaamini tamasha la mwaka huu litakuwa kubwa tofauti ya miaka miwili iliyopita toka lianzishwe Jijini Mwanza.
"Toka Lakwetu Concert lianzishwe tumeona ukuaji mkubwa wa tamasha, watu wameanza kutuelewa na kulipenda tamasha letu" alisema Bi Catherine.
"Mwaka huu tumeanza Maandalizi mapema Sana toka mwezi wa pili na hadi kilele chake tunaamini kusudi letu litakuwa limefikia hatua nzurii zaidi"
"Tumepita kwenye makanisa Saba Jijini Mwanza kwa kuandaa matamasha ya kuimba kwa kuzileta kwaya mbalimbali kutoka madhehebu yote, waimbaji wa bendi na waimbaji binafsi kwa ajili ya kumsifu Mungu pamoja na kujiandaa na kilele Cha tamasha letu la Grand Finale"
Bi Catherine alisema tamasha la finali la Lakwetu Concert litakuwa na Mambo Mbalimbali mazuri Sana kupita miaka miwili iliopita .
Alisema tamasha hilo litafanyika Katika Uwanja wa CCM Kirumba tarehe 9 Juni Mwaka huu kwa vikutanisha Vikundi zaidi ya arobaini kutoka Mikoa mbalimbali Nchini.
Pia watakuwepo washiriki wa Shindano la Rock City Gospel Search 2019 siku hiyo na watazamaji watapata nafasi ya kuwaona ili wawafahamu na kuviona vipaji walivyonavyo.
Tamasha la Lakwetu Concert ni Kongamano kubwa la Kuimba na kusifu lililobuniwa makusudi kuwaleta waimbaji wa Muziki wa Injili pamoja ili kumsifu Mungu kwa Nyimbo na tenzi, linalozunguka Mikoa mbalimbali Nchini.