Rais wa Venezuala Nicolas Maduro amevitolea wito vikosi vyake vya jeshi kujiweka tayari kwa hatua zozote za kijeshi kutoka Marekani wakati wafuasi wa kiongozi wa upinzani Juan Guaido wakikusanyika kwenye kambi za jeshi kujaribu kutafuta uungwaji mkono.
Maduro ameliamuru jeshi kujiandaa kuilinda nchi hiyo kwa kila zana zilizopo iwapo Marekani itajaribu kuchukua hatua za kijeshi katika taifa hilo la Amerika ya Kusini lenye utajrii mkubwa wa mafuta.
Katika kusisitiza kuwa juu ya jeshi linaendelea kuuunga mkono utawala wake wa kisoshalisti, Maduro alitoa hotuba kupitia televisheni akiwa pamoja na waziri wake wa ulinzi sambamba na vikosi vya kiasi wanajeshi 5,000
Harakati za Guaido zilipata uungwaji mpya jana Jumamosi kutoka kwa waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, alietoa ukanda wa vidio akiwahimiza raia wa Venezuela kuchukua hatua akisema wakati wa mabadiliko kwa taifa hilo ni sasa.
Marekani bado haijaondoa uwezekano wa kutumia hatua za kijeshi kumuondoa Maduro madarakani.
Social Plugin