Mahakama Kuu ya Tanzania imebatilisha sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi Mkuu.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Atuganile Ngwala kwenye kesi ya msingi namba 6 ya mwaka 2018 iliyofunguliwa na mtoto wa marehemu Chacha Wangwe ambaye ni Bob Chacha Wangwe.
Katika kesi hiyo ya Kikatiba, Jaji Ngwala amebatilisha vifungu viwili vya Katiba cha 7 (1) ambapo kinaeleza kuwa ‘Kila Mkurugenzi wa Jiji na Halmashauri wanakuwa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu’
Pia imebatilisha Kifungu cha 7 (3) kinachoeleza kuwa Tume inaweza kumchagua mtu yoyote kuwa msimamizi wa Uchaguzi wakati katiba inasema huwezi kuwa Mwanasiasa na ukawa msimamizi wa uchaguzi bali inatakiwa achaguliwe mtu huru.
Baada ya kueleza hayo, Jaji Ngwala amesema anazifuta sheria hizo na kama kuna upande haujaridhika ukate rufaa.