Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kerugoya kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamelazimika kuingilia kati na kutuliza hali baada ya wanawake wanne kujitokeza na kuanza kuzozania mwili wa mwendesha bodaboda.
Janet Wambui, Lydia Wanjiru, Susan Wakuthii, na mwingine wa nne kutoka kijiji cha Kimbimbi walifika katika hifadhi ya wafu hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kirinyaga kila mmoja akitaka kuuchukua mwili wa marehemu Peter Mwangi akidai ni mumewe.
Kizaazaa kilizuka pale ambapo kila mwanamke alidai kuwa mke halali wa marehemu na kutaka apatiwa fursa ya kumzika.
La kushangaza kila mwanamke alikuwa na mtoto wa kiume ambaye alijaliwa na marehemu aliyefariki dunia Jumapili Aprili 28 kwa njia isiyoeleweka.
Baada ya mvutano mkali kati ya wanne hao, familia ya marehemu iliamua kumzika marehemu nyumbani kwa mjomba wake ambapo hafla ya mazishi ilifanyika bila tatizo.
Chanzo - Tuko
Social Plugin