Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI IKUPA AIPIGA JEKI UWT DODOMA MIFUKO 30 YA SARUJI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Dodoma Rehema Mwendamaka alipowasili katika ofisi za chama kukabidhi Saruji Mifuko 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma Neema Majule akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa alipowasili katika ofisi za chama kukabidhi Saruji Mifuko 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya chama cha CCM mkoa wa Dodoma alipowasili kutoa mchango wake wa saruji mifuko 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto kushoto kwake ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma Neema Majule.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akikabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa UWT Mkoa wa Dodoma wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Rehema Mwendamaka (katikati) mwenye T.shirt nyeupe ni Kaimu katibu wa UWT Diana Madukwa na mwingine ni Mwenyekiti wa UWT Neema Majule wakipokea mifuko hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Mkoa wa Dodoma,Rehema Mwendamaka akimpongeza kwa moyo wa dhati Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Kaimu katibu wa UWT Mkoa wa Dodoma,Diana Madukwa akimshukuru Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma,Neema Majule akimpongeza na kumshukuru kwa Moyo wa dhati aliouonesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Mwenyekiti wa  UWT Mkoa wa Dodoma,Neema Majule akimsisitiza jambo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa UWT Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.
Sehemu ya ujenzi wa kituo cha watoto kinachojengwa ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa amekabidhi mifuko 30 ya saruji.
Mwenyekiti wa a UWT Mkoa wa Dodoma,Neema Majule pamoja na baadhi ya viongozi wakiagana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa mara baada ya kuwakabidhi Mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto.

Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog,Dodoma

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa ametoa mifuko ya Saruji 30 kwa Umoja wa Wanawake Tanzania mkoa wa Dodoma (UWT) ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na jumuiya hiyo za kujenga kituo cha kulelea watoto jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kukabidhi saruji hiyo Naibu Waziri huyo amesema kuwa anaupongeza uongozi wa UWT Mkoa w Dodoma kwa ubunifu mkubwa ambao wameendelea kuufanya ikiwemo wa kujenga kituo cha kulelea watoto ambacho sasa ni mardi ambao utakuwa mkubwa sana.

“Nampongeza sana Mwenyekiti pamoja na wale ambao anaambatana nao ,hivyo kutokanana na mradi huu naamini wataondokana na utegemezi”alisisitiza Mhe.Ikupa

Aidha amesema kuwa Saruji hiyo itawasaidia kuwasogeza ,lakini pia amewaomba wadau mbalimbali waweze kujitokeza kusaidia kwani bado UWT wanahitaji vifaa mbalimbli vya ujenzi kama vile Mabati,Mbao ,na vifaa vingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma Neema Majule alisema kuwa wanamshukuru Waziri Ikupa kwa kuwa na moyo wa kipekee kwa kuwaletea mifuko ya sumenti 30 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa 3.

“Kiukweli ametushangaza sana wanawake wa Dodoma kwa upendo wake wa dhati maana sikila mtu aliyenacho anatoa,hivyo mimi na mjumbe wangu wa kamati ya utekelezaji, bado tunaendelea kuwaomba wale wote wenye mapenzi mema na uwt waweze kujitokeza kuchangai kwani bado tunahitaji,Mabati,Malumalu,Madirisha na milango ili ujenzi uweze kukamilika”amesema Majule.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa Mradi huo ni wa ccm mkoa lakini utasaidia wilaya zote saba zilizopo Dodoma. “Na lengo letu mara baada ya mradi huu kuanza ambao utakuwa na thamani ya shilingi mil.200,utaweza kabisa kufanya UWT DODOMA kuwa endelevu na utasaidia kuweza kuweka miradi mingine kila wilaya ili wanawake waweze kupata vitega uchumi kila wilaya kwa kujitegemea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com