Watu mbalimbali wamezidi kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea usiku wa kuamkia leo.
Chini ni baadhi ya viongozi waliotuma salamu zao za pole kupitia mitandao.
Peter Msigwa: Haijalishi tunaishi muda gani hapa duniani, cha msingi unatoa mchango gani hapa duniani kabla ya kifo. Dr Mengi sio tu uliwavutia wengi ,bali uligusa sana maisha ya wengi , umetuonyesha kuziacha jamii zetu bora zaidi kuliko tulivyo zikuta. Is all about donation not duration. RIP
Maria Sarungi: Rest in Peace @regmengi 🙏🏽 Your contribution to the growth of our industries in #Tanzania remain indelible. Pumzika kwa amani na Mungu awape faraja wanafamilia na marafiki katika kipindi hiki kigumu
Faustine Ndugalile: Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mzee Reginald Mengi. Hivi karibuni tulikutana na kuongea kuhusu kuanzisha huduma ya stem cell therapy hapa nchini. Nitakukumbuka kwa ubunifu, uthubutu na kutosita kujaribu mambo mapya. Natoa pole kwa familia na IPPMEDIA. RIP Mzee Mengi
Makamu wa Rais, Samia Suluhu: Moja ya vitu ulivyotuachia ni ule wepesi wako wa kusaidia masuala ya kijamii, daima tutakukumbuka. #RIPReginaldMengi
Zitto Kabwe: Msiba mkubwa kwa Taifa na haswa kwa Familia ya Mzee @regmengi . Pole sana @JNtuyabaliwe na Watoto, The twins. Poleni sana Regina, Abdiel na familia nzima ya Makampuni ya IPP. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi mahala pema anapostahili
Nape Nnauye - Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako}Pumzika kwa Amani Dr. R.A Mengi.
Godbless Lema - Watu wanagopa kifo,kimsingi tunacho ogopa ni kuwahi kufa kwani kifo hakizuiliki,ktk maisha ni vyema kuishi maisha ya baraka na watu wote,ili utakapo tangulia maisha yako yaweze kuwa na thamani.Nina mshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dr R.Mengi,kwani alijua thamani ya ubinadamu
January Makamba - Pole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins - na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi.
Social Plugin