Mamia ya waombolezaji leo Alhamisi Mei 9, 2019 wamejitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dr. Reginald Mengi.
Baadhi ya waliofika kanisani hapo ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, mbunge wa kuteuliwa, Anne Kilango na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndo ataongoza ujumbe wa Serikali katika mazishi ya Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 Dubai, Falme za Kiarabu.
Social Plugin