Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, Riziki Lulida (CUF), amesema wananchi wa mkoa huo wanakuwa wafupi kwasababu ya kubeba mizigo kichwani kwa kukosa usafiri kupitia barabara.
Lulida ameyasema hayo bungeni bungeni leo Mei 10, ambapo amesema kuwa Mkoa huo umekuwa ukitengwa kila mwaka kwa kunyimwa miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwamo ya barabara.
Lulida ametolea mfano wa barabara za jimbo la Liwale kwamba hazikuwahi kujengwa kwa kiwango cha lami tangu serikali ya awamu ya kwanza.
“Mheshimiwa Naibu Spika kuna ubaguzi unafanywa na mawaziri katika kugawa miradi hapa nchini, huko Lindi Liwale tumekuwa kama Guantanamo, ninashauri Bunge tutengue kauli ya kuapa kwa kutumia biblia au quran, tutumie katiba badala ya hiyo misahafu kwa sababu hivyo vitabu havitaki uongo.
“Niwaambie huko Lindi mnazuia kangomba ya korosho wakati hamjengi barabara, wale wafanyabiashara wanaamua kupeleka magari yao hata kwa shida lakini mnawazuia kununua korosho, je mnataka watu wafanyeje, leo hii watu wa Lindi wamekuwa wafu
Social Plugin