Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP , Dkt Reginald Abraham Mengi (75) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Dk Mengi amefariki dunia akiwa jijini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Dk Mengi amefariki dunia akiwa jijini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Dr. Mengi alizaliwa katika kijiji cha Nkuu huko Machame, Kilimanjaro, Tanzania. Baba yake Mr. Abhraham Mengi alizaliwa Marangu, Kilimanjaro, Tanzania lakini baada ya babu yake kufariki ilitokea mivutano juu ya urithi hasa kwenye masuala ya ardhi alilazimika kuhamia Machame ambapo napo licha ya kukutana na changamoto nyingi lakini aliweza kukaa akatulia. Baba yake Mzee Abraham Mengi na mama yake Ndeekyo walibarikiwa watoto saba yeye Dr. Mengi akiwa kama mtoto wa tano kuzaliwa ambao ni Apaanisa, Elitira, Asanterabi, Karileni, Dr. Mengi mwenyewe, Evaresta na Benjamin.
Dr. Mengi alianza shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Katika maisha yake ya shule tukio kubwa analolikumbuka ni wakati shule yao ya Old Moshi ilipohamishwa kutoka Old Moshi, Kolila na kuhamia Moshi mjini.
Baada kumaliza shule ya sekondari alipata ufadhili wa KNCU(Kilimanjaro Native Cooperative Union), alikwenda Uingereza kuchukua masomo ya uhasibu. Dr. Reginald Mengi ni moja kati ya watanzania wa mwanzo kabisa kusoma UK, Scotland na kufanikiwa kuwa Mhasibu anayetambulika na Taasisi ya Wahasibu ya Uingereza na Walesi
Mwaka 1971 Reginald mengi alirudi Tanzania na kuajiriwa kwenye kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ambayo kwa sasa inajulikana kama Prince water house Cooper. Baada ya kufanya kazi muda mrefu kwenye kampuni hiyo akiwa kama chairman and partner mwaka 1989 aliondoka kwenye kampuni hiyo na kwenda kuanzisha kampuni yake. Dr. Reginald Abraham Mengi ni mwanzilishi, mmiliki na Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Limited na Taasisi ya teknolojia na ugunduzi ya IPP(IPP Institute of Technology and Innovation).
Kupitia kampuni yake hiyo Reginald Mengi aliweza kumiliki vyombo mbalimbali vya habari mfano kwa upande wa TV alimiliki ITV, EATV na Capital Tv na kwa upande wa Radio anamiliki Radio one, Capital radio na EATV radio. Dr. Reginald Mengi alimiliki magazeti kadhaa, mfano wa magazeti hayo ni Nipashe, kulikoni, Taifa letu , The Guardian , Financial time na Sunday observer.
Mwaka 1992 Dr. Mengi alianzisha makampuni mengi zaidi yaliyokuwa yanazalisha bidhaa mbalimbali za kawaida ambazo zilikuwa ni adimu sana kwa wakati huo. Alikuwa tayari anamiliki biashara kadhaa ambazo ni;- Tanzania Kalamu Company Limited, Anche-Mwedu Limited, Tanpack Industries Limited, Industrial Chemicals Limited ambacho baadaye ilibadili jina na kuitwa Bodycare Limited pamoja na Bonite Bottlers Limited.
-Mwaka 1981 Dr. Mengi alianzisha kampuni kubwa ya uwekezaji iliyokwenda kwa jina la Mengi Associates Limited ambayo mwaka 1988 ilibadili jina na kuitwa Industrial Projects Promotion Limited na baadaye IPP Limited. IPP Limited kwa sasa ni jina linalojulikana sana Tanzania. Dr. Mengi anasema karibia fedha yote anayotumia kuanzisha makampuni haya inatokana na faida inayopatikana katika kampuni zilizopo.
-Dr. Mengi alikuwa anasita sana kuwekeza katika vyombo vya habari kutokana na uhalisia wa mazingira ya kitanzania kisiasa lakini kufikia mwaka 1993 aliamua kuingia huko kwa kuanzisha Radio One, Itv kisha magazeti kama vile Nipashe, The Guardian n.k.
Reginald Mengi alimiliki viwanda baadhi ambavyo vinazalisha vinywaji mbalimbali hapa Tanzania. Alimiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji, Bonite Bottlers inayoongoza kwa kinywaji cha Coca-Cola na maji ya chupa ya Kilimanjaro. Dr. Mengi pia amewekeza katika madini, mafuta, gesi, gesi asilia, madawa, kilimo cha mboga mboga katika maeneo makubwa, magari(kuunganisha magari ya umeme), saruji na mambo mengine zaidi katika sekta ya utengenezaji(manufacturing sector).
Dr. Mengi amewahi pia kuwa katika nafasi kadhaa za uongozi wa umma ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa magazeti Tanzania(Chairperson of Tanzania Standard Newpapers); Kamishna wa kamati inayoshughulikia mishahara(Commissioner of Salary Review Commission); Mwenyekiti wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania(NBAA); Mwenyekiti wa Baraza la Taifa La Mazingira Tanzania(National Environmental Council of Tanzania(NEMC); Mwenyekiti wa Vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania(Chairman of the Tanzania Chapter Commonwealth Press Union(CPU)); Mkurugenzi wa bodi ya LEAD(Leadership for Environment and Development International); Kamishna wa kamati ya Ukimwi Tanzania (Commissioner of Tanzania Commission for AIDS(TACAIDS); Mwenyekiti wa Muungano wa viwanda Tanzania(Chairman of the Confederation of Tanzania Industries(CTI); Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki(Chairman of the East African Business Council); Mwenyekiti wa ICC Tanzania (a National Committee of the Intenational Chamber of Commerce); Na Mkurugenzi wa Bodi Ya Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola(Director of the Board of Commonwealth
Kuanzia mwaka 1987 Dr. Mengi amekuwa akisaidia upandaji miti kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa sababu amekuwa akiona msitu ukipungua katika mlima Kilimanjaro. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 zaidi ya miti milioni 24 ilikuwa imepandw. Kwa mchango huu katika mazingira, Rais Mkapa alimchagua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la kusimamia Mazingira Tanzania(NEMC)National Environmental Management Council licha ya kwamba anatokea katika sekta binafsi.
Dr. Mengi hadi mauti unamkuta alikuwa ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania(Chairman of the Media Owners Association of Tanzania(MOAT) na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania(the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)
Dr. Mengi alikuwa mtu anayejulikana sana kwa kutoa sana misaada ya kijamii(philanthropist). Amepewa tuzo mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa akitambulika sana kwa kazi yake ya kujitolea kwa watu. Amepewa tuzo ya “The Order of the United Republic of Tanzania” mwaka 1994 na “The Order of The Arusha Declaration of the First Class” zilizotolewa na Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995. Amepewa tuzo ya “The Martin Luther King Jr. Drum Major for Justice iliyotolewa na Marekani mwaka 2008. Amepewa tuzo ya “The International Order of the Lions Club iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Lions Club mwaka 2014; na “The 2012 Business For Peace Award” iliyotolewa na Taasisi ya Oslo Sweden ya “Business for Peace Foundation” baada ya kupendekezwa na kamati inayotoa tuzo za Nobeli.
Kwa kutambua juhudi zake za kupambana na rushwa na ufisadi nchini mwaka 2008 serikali ya Marekani ilimpatia tuzo ya “Martin Luther King Jr. Drum Major Award”
Mwaka 2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alimpatia Dr. Mengi tuzo ya taifa katika mambo ya kuisaida na kuiwezesha jamii hasa katika ujasiriamali wa kijamii “The National Philanthropy Award” katika sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mengi amefariki dunia akiwa kwenye matibabu Dubai, U.A.E, usiku wa kuamkia leo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu , mahali pema, peponi
Reginald Mengi alifiwa na aliyekuwa Mke wake wa kwanza, Mercy Mengi usiku wa kumkia November 1,2018.
Social Plugin