Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGODI WA NYAMONGO WAPIGWA FAINI YA BILIONI 5.6


Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), imeupiga faini ya shilini bilioni 5.6 mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, kwa kushindwa kudhibiti bwawa la maji yenye sumu na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wanaozunguka mgodi huo.

Maamuzi hayo yalitolewa jana baada ya Waziri wa Madini, Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kufanya ziara mgodini hapo, wakiambatana na Watendaji mbalimbali.

Faini hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka baada ya ripoti ya Kamati Huru iliyoundwa kwa ushirikiano wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) pamoja na Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam kubaini mgodi huo umekuwa ukitiririsha maji yenye sumu kwa zaidi ya miaka 10 huku ukitoa taarifa zenye udanganyifu kuhusiana na maji hayo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (kushoto), pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Kamati Huru iliyoundwa kuchunguza malalamiko ya utirishaji wa maji yenye sumu kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Sehemu ya eneo linalokusanya maji yenye sumu kwa ajili ya kuyasukuma kwa mashine kuyarudisha kwenye bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu katika mgodi wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko wakiwa wameambataba na viongozi mbalimbali kukagua mazingira mbalimbali yanayozunguka mgodi wa Acacia North Mara.
Viongozi hao wakijionea mtaro uliochimbwa na mgodi wa Acacia North Mara kwa ajili ya kunasa maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa la kuhifadhia maji/ tope sumu.
Sehemu ya maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa la maji yenye sumu kutoka mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Sehemu ya dimbwi la maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa (TFS) la kuhifadhia maji hayo.
Baadhi ya askari wanaoimarisha ulinzi katika mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Tazama Video hapa chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com