Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDALICHAKO AIPA KAZI NACTE


Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technologia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mkufunzi wa chuo cha Dare es saalam institute Technology juu ya kazi zinazofanyika chuoni hapo wakati wa maonyesho ya mabanda ya vyuo vya kati jijini Dodoma.
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji akionyesha namna ya kuzima moto, wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya nayofanyika Jijini Dodoma.
Msajili wa chuo cha Bandari cha Dar es Saalam wa kwanza kushoto, Jonneo Lugoye akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako juu ya kazi zinazofanywa na chuo hicho, wakati wa maonyesho kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia, Prof, Joyce Ndalichako katikati akiselebuka pamoja na msanii maarufu Mrisho Mpoto kushoto, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Tanzania Adolph Rutayuga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya huduma za kijamii, ambaye ni Mbunge wa jimbo la Chemba, Mh, Juma Nkamia akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Bw, John Kondoro akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Pro, Joyce Ndalichako akihutubia mamia ya washiriki wa ufunguzi wiki ya maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakati ya ufunguzi wa wiki ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

......................

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof. Joyce Ndalichako amelitaka baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Tanzania, NACTE, kujenga utamaduni wa kuvitembelea mara kwa mara vyuo vilivyo chini ya baraza hilo ili kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo hivyo iwe ya kiwango, ili kufikia malengo ya Serikali.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo, yaliyoandaliwa na baraza hilo yenye lengo la kuvikutanisha vyuo vilivyochini ya balaza hilo.

Amesema ni lazima NACTE ijenge utamaduni wa kuvitembelea vyuo hivyo ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayo saidia katika mkakati wa Serikali na kufikia malengo ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Amesema kama vyuo hivyo hazitatoa elimu na mafunzo bora lengo la kufikia nchi ya viwanda halitafanikiwa, ni wajibu wa baraza hilo kuhakikisha inasimamia utoaji wa mafunzo yaliyo bora.

“Pia niwatake ninyi baraza kama walezi wa hivi vyuo hebu mjenge utamaduni na tabia ya kuvitembelea vyuo hivyo vilivyochini yenu angalau vitoe elimu bora, kataka kufikia malengo ya serikali kufikia nchi ya viwanda, na tutafikia kwa kuhakikisha vyuo hizi vinatoa mafunzo bora” amesema Prof. Ndalichako.

Pia amesema serikali haitasita kukifungia chuo chochote kitakachokutwa kinaendeshwa kinyume na ithibati iliyotolewa na serikali, kwani itakuwa ni kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali.

Pia amevitaka vyuo hivyo kutumia maonyesho kubadilishana mawazo, na namna ya kutoa mafunzo bora na kukuza ushirikiano baina ya taasisi, wadau wa maendeleo pamoja na waajiri mbalimbali katika kuuza sekta hiyo.

Amesema katika kuhakikisha elimu hiyo inakuwa serikali kupitia wizara hiyo imetenga kiasi cha milioni kumi na nane(18,000,000) kujenga chuo kikubwa cha ufundi jijini Dodoma kitakachosaidia kukuza elimu ya ufindi, pia imetengwa bilion arobaini kujenga vyuo vingine ishirini na tano (25) maeneo mbalimbali.

Sambamba na hilo serikali imepanga kukarabati vyuo hamsini na nne(54) vya ufundi ili kufikia kutoa mafunzo yaliyobora, na kuongeza udahili wa wanafunzi wa ufundi mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa NACTE Adolph Rutayuga amesema tangu kuanzishwa kwa baraza hilo mwaka 1997 na kuanza rasmi kazi zake mwaka 2001 wamefanikiwa kudhibiti uanzishwaji wa vyuo vya ufundi kiholela.

Amesema jumla ya vyuo vyote ni mia tano arobaini(540) na kati ya hivyo mia mbili hamsini na moja ni vya umma na mia tatu kumi na tisa na vya binafsi na kati ya hivyo vyuo ishirini na moja havikukidhi matakwa na vilifutwa kabisa usajiri wake.

Maonyesho hayo yatakayo dumu kwa siku tano yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, umebebwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya ufundi na mafunzo kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda Tanzania”.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com