Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI NDITIYE AWATAKA WATANZANIA KUSOMA KWANZA MAELEKEZO YA TIKETI KABLA YA KUKATA TIKETI ILI KUONDOA MIGOGORO


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amewataka watanzania  Kuwa na desturi ya kusoma kwanza maelekezo yaliyopo kwenye tiketi  ya kusafiria  pindi wanapotaka kusafiri ili kuondoa migongano na migogoro baina yao na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri. 


Mhe.Nditiye ameyasema hayo Mei 30,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa ShauriMoyo  Mhe.Mattar Ali Salum  aliyehoji juu ya  baadhi ya kampuni za usafiri hususan Usafiri wa Majini kwa njia ya Boti  kuuza tiketi kwa abiria  kwa ajili ya Safari  lakini abiria anapochelewa safari tiketi hiyo  huwa haitumiki  na hivyo kusababisha hasara na usumbufu kwa abiria . 


Katika Majibu yake Mhe.Nditiye amesema tiketi ni moja ya mkataba kati ya abiria na mmiliki wa chombo cha usafiri hivyo abiria  anatakiwa kusoma kwanza maelekezo yaliyo kwenye tiketi na kama hatoridhika na maelekezo hayo ana ruksa ya kusitisha kukata tiketi ili kuondoa usumbufu.

Hata hivyo,Mhe.Nditiye amesema ufuatiliaji wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano  kupitia TASAC Umebaini kuhusu changamoto hizo na serikali inalifanyia uchunguzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com