Baada ya Video yenye utata inayoashiria kuwa na maudhui ya kingono ambayo inahusishwa na Askofu huyo, Jeshi la Polisi limefunguka kuwa limemuita ajieleze.
Kwa Mujibu wa Kamanda Mambosasa, Askofu Gwajima ameitwa Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na ataripoti kesho Mei 8,2019 saa tatu asubuhi
Ameongeza kuwa akichelewa atakamatwa na wamememuita sababu ingawa hakuna aliyelalamika lakini wameona ni kitendo cha ukiukwaji wa maadili, awe Askofu awe Mtu wa kawaida ule ni unyama
“Tayari Askofu Gwajima ameitwa Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na ataripoti kesho asubuhi, akichelewa atakamatwa na tumemuita sababu hakuna aliyelalamika lakini tumeona ni kitendo cha ukiukwaji wa maadili, awe Askofu awe Mtu wa kawaida ule ni unyama”,amesema Mambosasa
Social Plugin