Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OFISI YA CAG YAKAGULIWA, SPIKA NDUGAI ANENA


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema taarifa ya ukaguzi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imekamilika huku akisema ‘katika ukaguzi hakuna anayejikagua mwenyewe.’


Akitoa taarifa hiyo leo Alhamisi Mei 16, 2019, bungeni, Spika Ndugai amesema kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa umma, hesabu za ofisi ya CAG hupitiwa na Bunge kwa kuielekeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kufanya kazi hiyo.


 "Ningependa kuwajulisha juu ya taarifa ya  ukaguzi wa ofisi ya CAG kwa mwaka fedha unaoshia Juni, 2018, hesabu za CAG zinapaswa kukaguliwa walau mara moja kwa mwaka, PAC inajukumu la kukagua ofisi hiyo, kazi imeshafanyika na tumeletewa  taarifa," amesema.

Ameendelea kwa kusema kuwa, "Taarifa ya kukaguliwa ofisi ya CAG, nimeshaipitia kuna mambo, lakini kiutaratibu nimeshaipeleka PAC na wakishamaliza uchambuzi watawasilisha kwangu, niwataarifu kwenye masuala ya ukaguzi hakuna anayebaki kila watu wanawakagua wenzao,".



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com