MJAMZITO AJIPASUA TUMBO KUTOA MTOTO TUMBONI RUKWA

Mwanamke mmoja anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto, wilayani Nkasi mkoani Rukwa Kusini Magharibi mwa Tanzania.


Tukio hilo limevuta hisia za wengi na wengine wakiwa katika taharuki wengi wakifika katika kituo cha afya kushuhudia ukweli wa tukio hilo linalodaiwa kutekelezwa na bi Joyce Kalinda.

Wakati taarifa za awali zikisema kuwa mwanamke huyo alijipasua umbo, Mganga mkuu wa wiaya ya Nkasi Dokta Hashi Mvogogo alizungumza na gazeti la Habari Leo alisema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa kilichotokea kwa mama huyo.

Uchunguzi unafanyika kubaini kama alijifanyia upasuaj mwenyewe kutoa mtoto au kuna mtu mwingine alifanya hivyo.

Daktari huyo amesema saa tisa alfajiri ya kuamkia siku ya Alhamisi, mwanamke huyo alifika katika kituo cha afya cha Kirando na kuanza kupiga kelele, akimtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampe huduma za kumsaidia kujifungua.

Alisema kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo, muuguzi alimshauri mama huyo mja mzito kusubiri kidogo kisha alikwenda kumhudumia mgonjaw mwingine, lakini aliporejea mahali apokuwepo hakumkuta.

Kwa mujibu wa Dokta Mvogogo,ilipotimu alfajiri saa 11 mja mzito huyo alirudishwa hospitalini hapo akiwa amepasuka sehemu ya tumbo, huku watu waliomfikisha hospitalini hapo wakiwa wamembeba mtoto mchanga.

Watu hao walisema mwanamke huyo alikuwa amejipasua tumbo na kumtoa mtoto tumboni.

''Tumbo lilionekana limepasuliwa na kitu chenye ncha kali.Alipofika aliwekewa dripu tatu za damu ili kuokoa maisha yakekwani alikua amepoteza damu nyingi, lakini pia mtoto alipewa matibabu kutokana na kutolewa tumboni bila kufuata utaalamu unaotakiwa na sasa wote wanaendelea vizuri na matibabu,'' Dokta Mvogogo aliiambia Habari Leo.

Dokta Mvogogo amesema tukio hilo limeripotiwa polisi ili uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ni nini kilichotokea kwa mama huyo.

''Uchunguzi unaofanywa pia unahusisha mtaalamu wa magonjwa wa akili ambaye tunataka achunguze ili kubaini kama mama huyo ambaye huo ni uzao wake wa nane ana ugonjwa wa akili au la,'' alieleza Daktari huyo.

Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post