Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya mzungumzo na viongozi wa Iran, kama watamtafuta.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, Trump alisema anatarajia viongozi wa Iran wampigie simu.
Aidha rais huyo amesema kuwa aliamuru kupelekwa kundi la manowari zinazobeba ndege za kivita katika Ghuba ya Mashariki ya Kati kwa sababu ya vitisho vya Iran.
Mwaka jana, Trump alijiondoa kutoka mkataba wa nyuklia na Iran na kisha akaongeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kuwepo suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huo.
Hapo jana, viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walisisitiza kuhusu dhamira yao ya kuuheshimu muafaka huo wa mwaka wa 2015, lakini wakasisitiza kuwa hawatakubali masharti yoyote.
Social Plugin