Serikali iko mbioni kuanzisha program maalum ya magonjwa yasiyoambukiza kama ilivyo kwa magonjwa ya Ukimwi, TB na Marelia kwa kufikisha huduma ngazi ya zahanati.
Katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza wananchi wameshauriwa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki, kula mlo unaofaa, kutotumia tumbaku na pombe.
Hayo yameelezwa bungeni na Naibu waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile bungeni leo, Mei 17 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji (CCM).
Katika swali lake, Mwantum alitaka kujua serikali ina mpango gani kushughulikia magonjwa yasiyoambukiza kama vile, presha, kansa na kisukari.
Social Plugin