Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kupokea mashine 60 za kusafishia figo kutoka Nchini Saudi Arabia ambazo zitafungwa katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi.
Ameyasema hayo Leo Jumanne Mei 21 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (CCM).
Katika swali lake, Mwamoto amedai kwamba mashine za kusafishia figo zipo sehemu chache hapa nchini na wagonjwa wanapata shida.
Aidha Mbunge huyo amedai kwamba Serikali haioni kwamba umefika muda wa kila Hospitali ya Rufaa kuwa na Mashine ya kusafishia figo.
Akijibu swali hilo Ummy amekiri kuona ongezeko ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambapo amedai kwamba Serikali inatarajiwa kupata mashine 60 kutoka Serikali ya Saudi Arabia na kwamba changamoto ambayo itajitokeza ni ukosefu wa wataalamu lakini wameongea na Serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kupeleka wataalamu kwaajili ya kujifunza.
Social Plugin