Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MITAMBO YA KUTENGENEZEA SILAHA YAKAMATWA SINGIDA


Kikosi Kazi Cha Jeshi la Polisi Makao Makuu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Singida kimefanikiwa kukamata silaha aina ya gobore lililotengenezwa kienyeji pamoja na mitambo mbalimbali ya kutengenezea silaha.

Akiongea na waandishi wa Habari jana katika maeneo ya ofisi ya RPC Singida, Mkuu wa Oparesheni maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Mihayo K. Msikhela ameeleza kuwa mafanikio hayo yalipatikana siku ya tarehe 19.05.2019 Majira ya saa 3:30 usiku huko katika Kijiji cha nguvumali, Kata na Tarafa ya Ndago Wilayani Iramba ambapo zilipatikana taarifa za kiintelijensia zilizopelekea kukamatwa mtuhumiwa Hamisi Mohammed, (52), Mkazi wa Mtaa wa Nkulusi - Ndago ambaye alikutwa na silaha aina ya gobore na mitambo ya kutengenezea silaha.

Mihayo ameeleza kuwa msako ulieendelea na kukamatwa watuhumiwa wengine 6 ambao ni Mohammed

Hassan, (89) Mhunzi na mkazi wa Kijiji cha Nkingi - Misigiri , Kassim Mohamed, (34) mkazi wa Nkulusi - Ndago , Mkapa Msengi (47), mkazi wa Nguvumali - Ndago.

Amewataja wengine kuwa ni Hassan Hamis (28) , mkazi wa Nkulusi - Ndago, Idd Mohammed, (45), Mkulima na mkazi wa Ndago na Swaleh Ally , (49), mkazi wa Nkulusi Ndago.

Mkuu wa Oparesheni huyo amesema kuwa watuhumiwa wote 7 wanshikiliwa kwa mahojiano zaidi na baada ya mahojiano kukamilika watafikishwa Mahakani ambapo ametoa wito kwa wananchi wote hasa wenye mapenzi mema kuendelea kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu na viashiria vya uhalifu ili kuendelea kuifanya nchi iendelee kuwa salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com