Mabingwa watetezi Simba leo wamebeba pointi tatu mbele ya Ndanda FC na kuanza kunukia ubingwa wa ligi msimu huu kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Uhuru.
Meddie Kagere kipindi cha kwanza amepachika mabao yote mawili ambapo bao la kwanza amefunga dakika ya tatu akimalizia pasi ya John Bocco na bao lake la pili alifunga dakika ya 11 akimalizia pasi ya Clatous Chama.
Ushindi huo umewapa nafasi Simba kujikita kileleni wakiwa na jumla ya pointi 88 na wamebakiwa na michezo mitatu ili kukamilisha mzunguko wa pili.
Kwa nafasi ambayo kwa sasa Simba wamefikia wanahitaji pointi mbili ili kujihakikishia kutetea ubingwa wao msimu huu.
Simba wamepiga jumla ya mashuti 10 ambayo hayakulenga lango huku Ndanda wakipiga jumla ya mashuti sita ambayo hayakulenga lango.
Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Singida United utakaochezwa uwanja wa Namfua Mei 21.
Social Plugin