Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Harrison Mwakyembe (kulia) akitoa zawadi ya kikombe kwa mchezaji wa timu ya Sevilla mara baada ya kushinda mechi yao ya kirafiki na timu ya Simba SC uliofanyika May 23, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo ilikuwa imedhaminiwa na Kampuni ya SportPesa.
Wachezaji wa Simba SC na Sevilla ya Hispania wakifurahia pamoja mara baada ya kumaliza mechi yao ya kirafiki iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukitokea kwa juu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ameshindwa kujizuia kwa kushangilia kwa nguvu wakati vijana wake wakichapwa mabao 4-5 na Sevilla kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mo Dewji alishindwa kujizuia ni baada ya kufungwa bao la tatu na John Bocco aliyepokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere.
Mo Dewji aliyekuwa ameketi karibu na Mkurungezi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Abbas Tarimba alianza kushangilia kwa nguvu huku akirukaruka baada ya Simba kupata bao la tatu.
Mo Dewji alikuwa amesimama huku akirukaruka na kumpa mkono wa pongezi Tarimba.
Baada hapo Mo Dewji alikaa chini huku akionekana bado kuwa na furaha akiwapa mkono wa pongezi waliokuwa karibu yake.
Mo Dewji hakushangilia bao hilo peke yake kwa upande wa viongozi waliokuwa jukwaa Kuu ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Magori, Mwenyekiti Swedy Mkwabi.
Social Plugin