Wababe wa Simba msimu huu, Kagera Sugar ambao waliifunga Simba nje ndani na kuwa timu ya kwanza kubeba pointi sita leo wamepoteza mchezo wao mbele ya Stand United kwa kufungwa mabao 3-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Stand United walianza kucheka na nyavu mapema dakika ya 3 kipindi cha kwanza kupitia kwa Charles Chinonso kabla ya mshambuliaji machachari wa Kagera Sugar, Kassim Khamis kusawazisha bao hilo dakika ya 45.
Kipindi cha pili Jacob Masawe dakika ya 48 alipachika bao la pili kabla ya bao la tatu la ushindi kupachikwa dakika ya 90 na Datius Peter lililoipa pointi tatu timu yake ya Stand United.
Social Plugin