Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi na masomo zilizotangazwa na jumuiya za kimataifa kama ifuatavyo:
i. Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola;
Afisa Msaidizi wa Programu katika Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (Assistant Program Officer-Monitoring and Evaluation Unit na
Meneja wa Utafiti–Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Research Manager–Economic, Youth and Sustainable Development.
i. Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola;
Afisa Msaidizi wa Programu katika Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (Assistant Program Officer-Monitoring and Evaluation Unit na
Meneja wa Utafiti–Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Research Manager–Economic, Youth and Sustainable Development.
Maelezo kamili kuhusu nafasi hizi yanapatikana katika tovuti: http://thecommonwealth.org/jobs. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 23 Mei 2019.
Aidha, Jumuiya ya Madola imetangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree). Mwisho wa kuwasilisha maombi ya nafasi hizo zinazojulikana kama Queen Elizabeth Commonwealth Scholarship ni tarehe 26 Juni 2019.
Maelezo kuhusu taratibu za kuomba nafasi hizo yanapatikana kupitia tovuti: http://bit.ly/2Ytd8jJ.
ii Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR);
Kamishina Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Hifadhi kwa Wakimbizi (Assistant High Commissioner for Protection).
Maelezo kuhusu nafasi hii yanapatikana kupitia tovuti: https://www.unhcr.org/career-opportunities ambapo mwisho wa kuwasilisha mombi ni tarehe 20 Mei 2019 katika baruapepe recruitment.AHC-P@unhcr.org.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Social Plugin